MOVE COP 28 (Mobile Dustbin) Chini ya Shirika la PAWACAP
PAWACAP ORGANIZATION imesajiliwa kama shirika lisilo la kiserikali lifanyalo kazi zake za kuisaidia jamii zolizo athirika na mabadiliko ya tabia ya nchi hasa wafugaji nchini Tanzania. Shirika hili limeungana na kampuni ya Quality Water and Sanitation kuendesha mradi wa MOVE COP 28 wenye lengo la kukusanya takataka katika mikusanyiko ya watu kwenye makongamano makubwa.Kwa kutumia mfumo wa kuvaa kibebea taka inayotembea na wahudumu wetu yenye kauli mbiu naomba taka yako.
Lengo kuu la mradi huu ni kuzuia uchafuzi wa mazingira unao tokana na makongamano hayo, na pia mradi huu unatolewa bure kabisa na una fanya na taasisi za wazawa hapa nchini na lengo ni kuimarisha utunzaji wa mazingira na kuunga mkono juhudi za serikali katika eneo la utunzaji wa mazingira.
Hivyo wewe kama mdau muhimu katika utunzaji wa mazingira tunaomba udhamini katika eneo hili ili kuwezesha kupata vifaa vya kukusanyia takataka na mavazi maalum yatakayo valiwa wakati wa zoezi hili kama vile over roll na reflector.
MOVE COP 28 itatumia makongamano hayo kutangaza biashara na miradi ya wale wote watakao dhamini kwa kubandika mabango au nembo zao katika mavazi maalum yatakayo valiwa na timu yetu na pia kuwataja wadhamini katika vyombo vya ahabari tutakavyotumia kujitangaza.
Tunatanguliza shukrani zetu kuwa ombi letu litakubaliwa.